Kituo cha Nishati Kimeanzishwa kwa ajili ya kutoa huduma katika vijiji vyote vya Ngarenanyuki.
Kwenye Kituo cha Nishati vinapatikana vifaa vifuatavyo:
Tochi na taa ndogo za umemejua zenye uwezo wa kuchaji simu;
Mfumo mdogo ya umemejua, wa kiwango cha balbu 1 au 2 na chaja ya simu;
Mfumo wa umemejua wa kufunga kwenye paa la nyumba kwa ajili ya mwanga, chaja ya simu, redio. Pia unapatikana mfumo wa ngazi ya juu wa umeme tofauti na ule wa betri kwa ajili ya kutoa mwanga, kuendesha TV, kompyuta, nk .
Pia utapata:
Maelezo kuhusu teknolojia ya paneli za umemejua na matumizi yake;
Kuchagua mfumo unaokidhi mahitaji yako;
Msaada wa kiufundi kwa ajili ya mfumo wako wa umemejua;
Ufahamu wa kiufundi kuhusu kufunga paneli, matatizo madogo na ukarabati wa mfumo wa paneli;
Huduma ya mitambo ya gesi(biogas), majiko yaliyoboreshwa, sabuni za mmbono, mbogamboga zilizokaushwa, kompyuta na mtandao wa tovuti (internet) na barua pepe..