karibu kituo cha nishati

KITUO CHA NISHATI MBADALA KATA YA OLDONYOSAMBU:karibu kupata huduma ya nishati mbadala kituoni,mifumo ya paneli za umeme jua; saizi tofauti tofauti:-SOLATA inayochaji simu,TOCHI inayochaji betri. MGAHAWA KUTUMIA MAJIKO SANIFU,HUDUMA ZA COMPUTER,MAJIKO SANIFU NA BANIFU:-jiko janja,kapu la ajabu,MITI MICHE YA AINA MBALIMBALI INAPATIKANA:-parachichi, mibono,albizia, groton,moringa, markhmla, na mingineyo. MITAMBO YA GESI, SABUNI ZA MBONO JATROPHA, na USHAURI KEM KEM WA KUTOKA KWA MAMA NISHATI.

GHARAMA NA MAELEZO MENGINE

Bei ya Mfumo wa Paneli ya Umemejua inategemea idadi na aina ya vifaa vinavyotumiwa, na muda (masaa) vifaa hivyo vinategemewa kutumika.
Karibu Kituo cha Nishati kuongea na fundi wa umemejua kuhusu tathmini ya mifumo ya umemejua!

ZINGATIA: USHAURI MUHIMU!

Hakuna kivuli katika paneli: hata jani au kinyesi cha ndege kikianguka juu yake, kitapunguza uzalishaji wa umeme, Hakikisha katika mfumo wa umemejua kuna kirekibishi chaja: vinginevyo utaharibu Betri yako haraka!Usijaribu hata mara moja kuweka betri au paneli za aina na viwango tofauti: hii itapunguza ubora wa mfumo wako Usitumie betri za gari katika uzalishaji wa umeme jua: ni rahisi lakini ni mbaya kwa mfumo wa umemejua,Ukitumia betri inayotumia maji unaongeza maji ya baridi (distilled) kila yanapopungua (kmf mara 2kwa mwezi)Tumia nyaya za ukubwa ulio sahihi.Tumia fundi mzuri na mwelewa wa umemejua kutatua tatizo kutoka Kituo cha Nishati.