FAIDA:
1. Unatoa mwanga wa kutosha kunapokuwa na giza;
2. Huepusha magonjwa ya kupumua yanayosabishwa na taa zinazotumia mafuta ya taa ;
3. Unatoa fursa ya kuchaji simu na kusikiliza redio;
4. Ni teknolojia ya uhakika ;
5. Unahitaji ukarabati mdogo na rahisi;
6. Unaweza kuubadilisha kwa kuongeza paneli au betri baadae.
HASARA:
1. Gharama za awali ni kubwa lakini hulipa kwa kuzingatia fursa ya kulinda afya na kuokoa pesa baada ya muda kama mwaka mmoja;
2. Mfumo unahitaji kugharamia kirekibishi kwa vifaa vinavyotumia umeme usio wa Volti 12 (Chaja za simu, redio,…);
3. Vifaa vinavyotumia Volti 220 (TV, Friji) vinahitaji kirekibishi kingine kinachoitwa Inveta, kubadili Umeme wa DC kuwa AC.